YAFAHAMU MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA KIFO WAKATI WA TENDO - Fabiani 255

Fabiani 255

Jisomee Makala za Afya na Mapenzi Kila Siku

Friday, May 13, 2022

YAFAHAMU MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA KIFO WAKATI WA TENDO

MATUKIO ya watu kupoteza maisha ghafla wakati wa tendo, yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara lakini ni wachache wanaoweza kuwa wanajua ni nini husababisha tatizo hili huku wahanga wakubwa wakiwa ni wanaume.

Kiasili, tendo la ndoa limeumbwa kwa ajili ya kuwafurahisha wanandoa na kuzaliana, yanapotokea matukio ya watu kufa wakati wa tendo, watu wengi huanza kuogopa na wengine kuishia kupata misukosuko kutoka kwenye vyombo vya dola, vifo hivyo vikihusishwa na ukatili wa kijinsia, jambo ambalo mara nyingi huwa si sahihi.

Wataalamu wa masuala ya afya, wamefanya utafiti na kuja na sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha mtu akapoteza maisha ghafla wakati wa tendo la ndoa kama ifuatavyo:

1. MATUMIZI MABAYA YA DAWA
Wanaume mara nyingi hutumia dawa za kitamaduni, za mitishamba ili kuwasaidia kuwa thabiti wakati wa tendo hilo. Wengine huzichanganya na pombe wakiamini kuwa zitawasaidia katika kuongeza nguvu za kiume na hivyo kuwa na uwezo wa kujamiiana kwa ufanisi zaidi.

Wakati mwingine, baadhi ya wanaume huvuta sigara, hutumia dawa za hospitali bila maelekezo ya daktari na kutumia mihadarati ili kuongeza nguvu zao za kiume.

Wasichokijua wengi ni kwamba dawa zinazoaminika kuongeza nguvu za kiume, nyingi huwa na kemikali iitwayo ‘Nitrate’ (Naitreti), ambayo inaweza kusababisha shinikizo la damu na kusababisha kifo cha ghafla wakati wa tendo hilo.

2. MARADHI YA MOYO
Matatizo ya kiafya sio jambo linalopaswa kupuuzwa inapokuja katika suala la kushiriki mapenzi. Mtu mwenye historia ya ugonjwa wa moyo anaweza kufa wakati wa tendo hilo kwa sababu moyo wake utafanya kazi ngumu kuliko kawaida wakati wa kawaida.

Sababu za mara kwa mara za magonjwa ya moyo, hususani kwa wanawake wenye zaidi ya miaka 50 na wanaume wenye miaka arobaini ni shinikizo la damu, uvutaji wa sigara, kisukari, kiharusi na magonjwa mengine. Sababu nyingine ambayo mara nyingi husababisha magonjwa ya moyo ni msongo mkubwa wa mawazo.

Mshtuko wa moyo wakati wa tendo la ndoa mara nyingi huwakumba wanaume kuliko wanawake kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanyika. Hata hivyo, idadi ya watu wenye matatizo ya moyo ambao hupoteza maisha wakati wa tendo, huwa ni ndogo.

Utafiti unaonesha kwamba ni visa 34 tu vya mshtuko wa moyo kati ya 4,557 hutokea wakati au ndani ya saa moja ya kujamiiana na 32 ya wale walioathiriwa walikuwa wanaume.

Sumeet Chugh mtaalamu wa afya kutoka Taasisi ya Moyo ya Cedars-Sinai Heart Institute alisema utafiti wake ni wa kwanza kutathmini shughuli za kujamiiana kama sababu inayoweza kusababisha mshutuko wa moyo na utafiti wake ulichapishwa katika ripoti ya BBC Novemba mwaka wa 2017.

Utafiti wake huo uliwasilishwa katika mkutano wa American Heart Association wakati wa kutathmini vichocheo vinavyosababisha mshtuko wa moyo.

Sehemu ya maelezo yake inasema mtu huweza kupoteza maisha wakati wa tendo endapo moyo utapata matatizo na kuacha kupiga, jambo ambalo husababisha mtu kupoteza fahamu na kushindwa kupumua na iwapo hatapewa huduma ya kwanza kwa haraka, uwezekano mkubwa ni kwamba atapoteza maisha.

3. MATUMIZI YA KUPINDUKIA YA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME
Sababu nyingine inatajwa kuwa ni matumizi ya kupindukia ya dawa za kuongeza nguvu za kiume kama Viagra. Dawa hizi zimekuwa zikiuzwa katika maduka mbalimbali ya dawa duniani, kwa lengo la kuwasaidia wanaume hususan wenye magonjwa yaliyoathiri nguvu zao za kiume kuweza kurejesha uwezo huo.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, dawa hii inapaswa kutolewa na daktari kwa vipimo vinavyohitajika kulingana na tatizo lenyewe la kiafya.

Hata hivyo, kutokana na upatikanaji kwa njia rahisi wa dawa hizi, baadhi ya vijana na wanaume wamekuwa wakizinunua kiholela kwenye maduka ya dawa na kuzitumia ili kuwaridhisha wapenzi wao.

Kwa mujibu wa wataalam wa afya, matumizi yasiyofaa ya dawa hizi yanaweza kusababisha matatizo ya moyo na hivyo kuchochea kutokea kwa kifo wakati wa tendo hilo.

LIKE UKURASA HUU UKITUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK USIPITWE MAKALA NA MENGINE MENGI

AHSANTE KWA MUDA WAKO, NAOMBA SAPOTI KAZI YANGU KWA KUTAZAMA VIDEO HII MPAKA MWISHO

KWA TELEGRAM👇BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment