KUBUSIANA NI ZAIDI YA MSWAKI KIAFYA - Fabiani 255

Fabiani 255

Jisomee Makala za Afya na Mapenzi Kila Siku

Wednesday, May 11, 2022

KUBUSIANA NI ZAIDI YA MSWAKI KIAFYA

DAKTARI bingwa wa meno kutoka nchini Uingereza anasema watu wanapaswa kubusiana dakika 4 kwa siku ili kudumisha afya ya meno, lakini aliongeza kuwa kupigana busu si sawa hata kidogo na kupiga mswaki mara kwa mara na hakuna mbadala wake katika tiba ya afya ya kinywa ukilinganisha na kubigana busu kwa dakika nne mfululizo.

Watu wanapaswa kuongeza kupigana mabusu na kubembelezana kimahaba kwa dakika nne katika utaratibu wao wa kila siku ili kuongeza uzalishaji wa mate na kuosha bakteria wabaya waliokwama kwenye meno yao daktari bingwa alisema.

‘Mate ni muhimu kwa sababu hukusaidia kutafuna, kuonja, kumeza, kupigana na vijidudu mdomoni mwako na kuzuia harufu mbaya ya kinywa – jambo ambalo ni bora wakati wa kubusu.’

Mate pia hupunguza asidi ambayo hukaa kwenye meno yako, na kusaidia kupunguza hatari yako ya kuoza kwa meno.

Kubusu kunaweza kusaidia kuweka sawa afya ya meno yako na kuzuia harufu mbaya ya kinywa, alisema Daktari Khaled Kasem.

LIKE UKURASA HUU UKITUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK USIPITWE MAKALA NA MENGINE MENGI

AHSANTE KWA MUDA WAKO, NAOMBA SAPOTI KAZI YANGU KWA KUTAZAMA VIDEO HII MPAKA MWISHO

KWA TELEGRAM👇BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment