JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE - Fabiani 255

Fabiani 255

Jisomee Makala za Afya na Mapenzi Kila Siku

Tuesday, December 21, 2021

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE

Zamani ukimuuliza mtu unapenda upate mtoto gani wengi wao wangejibu mtoto wa kiume. Lakini hivi karibuni mambo yamebadilika watu wengi wanatamani kupata watoto wa kike zaidi kuliko wa kiume, wengine hutamani kupata mtoto wa kike baada ya kuwa na watoto wengi wa kiume.

Haijalishi ni sababu gani inakusukuma kupata mtoto huyo wa kike, pengine sasa umekuwa ukihangaika kutafuta njia rahisi ya kukusaidia kufanikisha azma yako hiyo. Basi Leo utakwenda kupata jibu lake, kwa kawaida yapo mambo matatu makubwa unayotakiwa kuzingatia ili uweze kufanikisha kwa haraka

1. Muda wa Kushiriki Tendo
Mwanaume hutoa mbegu za aina 2, X zinazotengeneza mtoto wa Kike na Y zinazoleta mtoto wa Kiume. Mbegu X huwa zinaishi muda mrefu zaidi zaidi kuliko Y hivyo basi ili kuweza kufanikisha kupata mtoto wa kike mapema inatakiwa kushiriki tendo la ndoa siku 2 hadi 4 kabla ya siku ya kutungisha mimba. Hii itasaidia mbegu hizi za X ziweze kuingia pindi tu yai linapotoka.

2. Mikao/Staili za kushiriki tendo la ndoa.
Mikao unayotumia wakati wa kushiriki tendo la ndoa inaweza kuathiri jinsia ya mtoto umtakae… Kwa kawaida epuka kutumia mikao inayoruhusu mwanaume kumwagia mbegu zake karibu kabisa na mlango wa kizazi. Hivyo pendelea zile staili ambazo mashine ya mwanaume haiingii ndani sana, mfano staili ya kifo cha mende.

3. Usimfikishe Mwanamke Kileleni.
Wakati mwanamke anafika kileleni huwa kuna ute fulani anautoa unaozisaidia mbegu za kiume kukimbia haraka na kuishi muda mrefu, ili kuondoa uwezekano huu wa kupata mtoto wa kiume basi ni vema kushiriki tendo la ndoa kwa kawaida bila mwanamke kufika kileleni.

NAAMINI UMEELIMIKA KAMA LILIVYOKUWA LENGO LANGU, SASA NAOMBA SAPOTI KWA KUTAZAMA TU HII VIDEO MPAKA MWISHO
KWA MAONI NA USHAURI NIANDIKIE HAPA
Inbox: Messenger

No comments:

Post a Comment